Latest Posts

WAWATA PAROKIA YA MT.JOSEPH MFANYAKAZI TARIME WAFANYA JAMBO KUBWA KWENYE PAROKIA YA MT. KIZITO WATUMIA 1,495,000

Na Helena Magabe Tarime.

 

 Wanawake Wakatoriki Tanzania (WAWATA) kutoka Kanisa kuu la Parokia ya Mt.Joseph mfanyakazi lililopo Tarime Mjini leo Machi 16,2025 ikiwa ni misa ya domika ya pili Wametumia 1,095,000 kununua vitu kwenye kanisa la Parokia ya Mt Kizito huku wakifanya harambee na kupata 400,000 jumla 1,495,000.

 

 Mwenyekiti wa WAWATA Parokia ya Tarime Mjini Veronika Malicha amesema umenunua vigae na madirisha 2 vyote thamani yake 880,000,sahani dazani 1 shilingi 40,000,Pazia 2 shilingi 100,000 mabomba 2 ya pazia shilingi 11,000,vijiko vya kusevia chakula 20,000,vikombe dazani 1,30,000 pamoja na vijiko vya chakula dazani 1 shilling 14,000 vitu vyote vyote hivyo vimeghalimu jumla 1,095,000.

 

Vitu hivyo vimekabidhiwa kwa Padre Japhet Swai Mkuu wa parokia ya Rebu Kanisa la Mt Kizito , lakini mbali na hilo Mwenyekiti Malicha amefanya harambee kwa shirikiana na uongozi wa WAWATA wa parokia hiyo na kufanikiwa kupata 400,000 ambazo amekabidhiwa padre huyo.

 

Padre Japhet Swai amewashuku WAWATA kwa tendo jema ambalo wamelifanya na kuwaomba Wakristo kujitoa kama Petro alivyomwambia Yesu kuwa wajenge vibanda tu vitatu kimoja cha Yesu, kingine cha Mussa na kingine cha Elia na kuongeza kuwa Wakristo wanaalikwa kujenga vibanda vitatu na kwamba tendo jema lililofanywa na WAWATA leo Wamejenga vibanda vitatu.

 

” Asanteni sana WAWATA Mungu awabariki sasa hivi hakuna baridi tangu tumeweka madirisha na sasa tutaweka dirisha jikoni ” alisema Padre Swai

 

Amesema kuwa hasira ya Mungu huamushwa na mambo matatu ambayo Mwanadamu anatakiwa kuyatekeleza ili hasira za Mungu zisiwake juu yake jambo la kwanza ni ugumu wa mioyo la pili tutomcha Mungu na jambo la tatu ni kuwa na juhudi ambazo hazina upendo.

 

Katibu Msaidizi na Muhazini wa WAWATA Parokia ya Mt.Joseph Mfanyakazi Amina Joseph Komba amewaomba kina Mama kujitoa bila kujibakiza kwani kutoa kwa Mungu kuna faida na kuongeza kuwa awali walichangia madirisha mawili ya nyumba ya Padre likabaki dirisha moja la jikoni ambalo wamemalizia leo.

 

” tulichangia madirisha mawili likabaki moja la jikoni ile mvua ya Jana lilipitisha maji leo tumamaliza waweke nawashauri kina mama wajitoe bila kujibakiza wengine wanafikiri pengine pesa zao zinaliwa na viongozi lakini sio kweli wewe toa, Mungu ataona umetoa mfano mzuri ni mimi mwenyewe leo nilikuwa na 2000 tu ya sadaka lakini nimetumiwa hela kwenye simu” alisema Komba

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!