Latest Posts

WAZAZI WAMESISITIZWA KUWEKA JITIHADA KWENYE MALEZI

 

Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Mtwara (JUWAM) limeendelea kutoa elimu kwa wanawake zaidi ya 200 kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo ukatili wa kijinsia pamoja na makuzi ya mtoto katika kijiji cha kawawa kata ya Mkunwa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu hiyo hasa makuzi ya mtoto Mwenyekiti wa jukwaa hilo la Wanawake,  Mariamu Chimbwahi amesema makuzi ya mtoto yanaanzia tangu mtoto akiwa tumboni kwa mama kabla hajazaliwa.

Elimu hiyo imetolewa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, elimu iliyotolewa katika kijiji hicho cha kawawa kata ya Mkunwa kwenye halmashauri hiyo.

Hata hivyo makuzi yanategemea namna ambayo wazazi wanawalea watoto hivyo wamesisitizwa kuweka jitihada kwenye malezi bora ya mtoto ili aweze kukua katika misingi ya kimaadili kinyume na hapo anakuwa akiwa na tabia isiyokuwa njema na baadhi yao kujiingiza katika vitendo vihofu kama vile matumizi ya madawa ya kulevya.

‘’Na suala la malezi siyo tu jukumu la mama pekee bali hata  akina baba kwahiyo tujitahidi kushirikiana na wazazi wenzetu kuwalea watoto wetu katika makuzi mazuri kwakuwa hakuna mzazi ambaye anataka mtoto wake akizaliwa awe na tabia mbaya, kila mzazi anataka mtoto wake awe na tabia mzuri kuanzia nyumbani hadi shuleni.’’Amesema Chimbwahi

Katibu wa Jukwaa hilo la Wanawake, Judith Chitanda amezungumzia suala la vitendo vya ukatili vinavyofanywa na  baadhi ya watu katika jamii yao hivyo amewaomba wanawake hao kuwa, kutofumbia macho pale wanapoona vitendo hivyo vikifanyika kwenye jamii.

‘’Akina mama ninyi wenyewe mnajua watoto wetu wanabakwa na kulawitiwa, kikubwa tumeona tuje kwenu kwasababu akina mama ndiyo walezi kwahiyo lazima tuzingatie malezi ya watoto  tunapoona vitendo hivi lazima tuviripoti, vikiripotiwa wengine wanaotamani kuvifanya hawawezi wataongopa.’’Amesema Chitanda

Mmoja wa wanawake hao akiwemo Betina Endrick mkazi wa kijijini hapo, amelipongeza jukwaa hilo kwa kuwaletea elimu hiyo ya malezi bora kwa watoto ambayo itaenda kuwasaidia katika kuwalea watoto wao lakini pia wataripoti vitendo vya ukatili vitapojitokeza kwenye jamii yao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!