Latest Posts

WAZIRI MHAGAMA: TUMIENI ZAHANATI HII VIZURI, MUITUNZE IENDELEE KUWASAIDIA

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amewataka wananchi wa kijiji cha Simbadamalu kilichopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Uyui Mkoani Tabora kuitumia zahanati ya kijiji hicho kwa kwenda kliniki pindi wakina mama wakiwa wajawazito pamoja na kuitunza ili iendelee kutoa huduma za afya.

Waziri Mhagama ametoa wito huo leo Desemba 21, 2024 wakati akizindua zahanati ya Simbodamalu pamoja na wodi ya mama na mtoto iliyopo katika kata ya Lutende ambayo itasaidia kutoa huduma za afya katika kijiji hicho.

“Wakina mama tumieni zahanati hii kwa kuja kupata huduma za kliniki mnapokuwa wajawazito ili tuendele kupunguza vifo kwa akina mama na watoto pamoja na magonjwa ya fistula kwa kuwa hii ni dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,” amesema Waziri Mhagama

Aidha, Waziri Mhagama wakati akiwa katika wodi ya mama na watoto iliyopo katika kata ya Lutende kijijini hapo, ameahidi kuchagia vitanda vinne vya kisasa vya kujifungulia wajawazito, magodoro, pamoja na mashuka ili huduma ziendelee kutolewa katika wodi hiyo.

“Tunataka kuona wananchi wetu kutoka kwenye kijiji hiki wanapata huduma za afya zenye viwango vya hali ya juu na sisi kama Serikali na mimi kama Waziri mwenye dhamani katika sekta ya afya nitaleta hapa vitanda vinne, magodoro na mashuka ili wakina mama wanapotoka kujifungua walale sehemu salama,” amesema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama baada ya kukagua nyumba ya mganga katika Kituo cha Afya Lutende amewaomba tena wadau wa sekta ya afya ambao ni Shirika la Kimataifa la World Vision Tanzania kuongeza milioni 50 ili ujenzi ukamilike pindi inapotokea changamoto yoyote kwa muda wowote, daktari awepo karibu na eneo la kazi.

Zahanati hiyo ya Simbodamalu pamoja na wodi ya mama na mtoto iliyopo katika kata ya Lutende zimejengwa kwa ushirikiano wa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wananchi pamoja na wadau wa sekta ya afya ambao ni World Vision-Tanzania.

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama amewaahidi wananchi wa kijiji hicho kuwaletea gari la wagonjwa (Ambulance) ili kurahisisha huduma za dharura hasa za wakina mama wajawazito pindi zitakapohitajika kwakuwa dhamira ya Rais Dkt. Samia ni kuona afya za wananchi wake zina imarika.

Waziri Mhagama ameishukuru World Vision- Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono Tanzania hasa katika sekta ya afya na kuwaomba wadau wengine kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa kuwa milango ipo wazi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!