Na Theophilida Felician, Kagera.
Viongozi wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania SHIVYAWATA kwa mkoa Kagera wameshukuru na kupongeza mchango wa aliye kuwa mbunge wa viti maalum kupitia asasi za kiraia NGOs Neema Lugangira kwa namna alivyokuwa karibu na kundi la watu wenye ulemavu mkoani Kagera.
Baadhi ya viongozi hao wakiwa ofisini kwao maeneo ya ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha wasioona TLB mkoa Annalise Lubago wamesema Neema akiwa katika uongozi lhakuwasahau bali alishirikiana nao mambo tofautitofauti hususani kuwashika mkono pale walipokuwa na uhitaji wa vitu muhimu.

Mwenyekiti Lubago amesema yeye binafsi aliwahi kumsaidia baada ya kijana wake aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha ualimu mpwapwa baada ya kukwama kupata Sh 250000 alimpatia taarifa hiyo Neema na hakukawia kumsaidia akalipa fedha hiyo.
Ameeleza kwamba licha ya kutokubahatika kupata nafasi hiyo tena wanaimani bado ataendelea kuwa nao kwa ukaribu katika ushirikiano.
Naye Novati Joseph Mwijage Mwenyekiti SHIVYAWATA manispaa ya Bukoba amefafanua kuwa mchango wa mbunge huyo uliwagusa kama kundi, mtu mmoja mmoja jambo lililowatia faraja sana.

Hata hivyo viongozi hao kwa pamoja wameyataja mengi likiwemo tukio la kuwanunulia ng’ombe na kumpeleka ofisini kwao kwa ajiri ya kitoweo kwa kila mtu mnamo tarehe 14 Juni 2025.
Wamehitimisha wakimuombea heri katika safari ya majukumu kwani ni mtu mpambanaji kupitia njia mbalimbali huku wakimsihi kutokukata tamaa baada ya kura za kuwania nafasi hiyo ya ubunge awamu nyingine kutokutosha kwake.