Latest Posts

ZAIDI YA BILIONI 12 ZIMETOLEWA KWAAJILI YA WANAWAKE MOROGORO

Serikali ya Mkoa wa Morogoro imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 12 kwenye vikundi 440 ambapo imehusisha wafanyabiashara 7411 waliosajiliwa ili kuwawezesha wanawake na wasichana kukuza uchumi wao na familia zao.

Hayo yamebainishwa leo Machi 8, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika katika Halmashauri ya Ifakara Mji, yakihimiza haki, usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maisha.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wolaya amesema kila taasisi zinawajibu wa kutoa elimu ili kuepukana na matukio maouvu ya ukatili wa kijinsia yakiwemo ubakaji na ulawiti hivyo wanapaswa kuvikemea vitendo hivyo ili kutunza maadili katika jamii.

Akisoma rusala katika maadhimisho hayo Rosemary Ngonyani amesema wanawake wameonesha umahiri kwenye kuchukua mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3, kupitia mfuko wa 10% ya mapato ya Halmashauri na mikopo mingine inayolenga kuimarisha uchumi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abubakar Asenga amekemea vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake huku akiwataka wanawake na wasichana kufika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya pale wanapofanyiwa vitendo hivyo ili sheria kufuata mkondo wake.

Naye, Apaa Mwabena mratibu wa miradi kutoka shirika la USWIS amesema wamekuwa katika mstari wa mbele katika kuwawezesha wanawake katika ufundi stadi ili kupata ajira na kujikwamua kimaisha.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!