Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) limekabidhi vifaa vya michezo vilivyotumika katika mashindano ya michezo ya Majeshi yaliyomalizika Septemba 15 mkoani Morogoro kwa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Lengo la makabidhiano haya ni kuhakikisha kwamba vifaa hivyo vinatumika kukuza na kuendeleza michezo katika chuo hicho na kwa jumla katika eneo hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania, Brigedia Jenerali Said Hamis Saidi, akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya SUA na kueleza kwamba baraza lina utamaduni wa kuacha vifaa kama alama katika Mkoa ambapo mashindano yalipofanyika,Vifaa hivyo vinatarajiwa kusaidia kukuza michezo katika chuo hicho na katika maandalizi ya mashindano ya SHIMIWI yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Septemba 15, uwanja wa Jamhuri Morogoro ulishuhudia hitimisho la mashindano ya BAMMATA, yaliyodumu kwa takribani siku 14 katika viwanja mbalimbali,Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kilikuwa moja ya taasisi ambazo viwanja vyake vilitumika katika mashindano hayo.