Latest Posts

SAID CHAMBIRI ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE TARIME MJINI

Na Helena Magabe -Tarime

‎Said Kisyeri Werema Chambiri Kijana Msomi wa aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Tarime Kiseryi Werema Chambiri jana  alichukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Tarime mjini  huku akibainisha  mambo yaliyomsukuma kuwania nafasi hiyo endapi atapata  ridhaa hiyo.

‎Akizungumza na Jambo tv kwa njia ya simu jana 30,2025 jioni alisema  kuwa  yeye ni mzaliwa wa Tarime aliyekulia na kusomea Tarime na hata Mungu alipombariki akapata ajira aliamua kurudi na kuwekeza Tarime biashara zake kadhaa  kwaajili ya kushirikiana na wananchi hivyo anayajua vizuri matatizo na changamoto za wanakazi wa Tarime Mjini  akipata ridhaa ya kuwa Mbunge wao atawawakilisha vema kwa kuyasemea matatizo yao  kwa sababu Mbunge ni kiunganishi kati ya Serikali na Wananchi.

‎Chambiri alibainisha kuwa  Tarime inahitaji Mtu mwenye maono, mwenye  ushawishi  na mwenye  uwezo wa kuunganisha fursa zilizopo Tarime kwani Tarime inatakiwa kuwa sehemu nzuri ya utalii huku akitolea mfano uwanja  wa ndege ulipo nkende kuwa msimu high season ndege zinatua pale zaidi ya 20 na gari za kitalii zinajaa  Tarime kiasi cha nyumba nyingi za wageni kujaa wageni ambao ni madereva wanachukua watalii uwanja wa nkende na kuwapeleka Serengeti.

‎Akiendelea kuzungumza alisema  amepata msukumo huo kwa sababu Tarime kuna fursa nyingi za maendeleo na kwa sababu ameishi kwenye utamaduni wa siasa muda mrefu anaona umefika wakati  wa yeye kuwa daraja na kiunganishi baina ya Wananchi na Serikali vilevile baina ya wanananchi na chama cha Mapinduzi CCM ilin kisigombanishwe  kwa sababu ndicho chenye dora .

‎Aidha aliongeza kuwa  licha ya kuwa mengi yamefanyila lakini  bado kuna mapungufu  hivyo Serikali inahitaji watu wenye maono watakao msaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe  Dkt Samia suluhu Hassan  hivyo akipata ridhaa atakuwa kiunganishi kwa kukisemea chama kwa ubora wake na kuwasemea Wananchi kwani Mbunge ana jukumu kubwa kwa kupeleka malalamiko ya Wananchi kwa serikali ili iyasikilize na kuyafanyia kazi.

‎Alifafanua kuwa Serikali haiwezi kupata malalamiko bila Mbunge kufanya mikutano ya mara kwa mara na  Wananchi na kusikiliza kero zao kwa kuwa muda wake mwingi anautumia akiwa Tarime atafanya mikutano ili kusikiliza kero na mahitaji ya wananchi na kuongeza kuwa Tarime ni Mji anaoupenda kuliko sehemu yoyote ile  Tanzania.

‎Hata hivyo   alisema Ilani iliyozinduliwa ni bora  imebeba mambo mengi mazuri hivyo inahitaji watayoisimamia vizuri kwaajili ya kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa Mheshimiwa Rais Dkt Samia  Suhulu Hassan hivyo chama kinahitaji zaidi viongozi wenye maono na kuongeza kuwa bila mahusiano mazuri na watendajibwa Serikali kama vile Mkuu wa Wilaya,Katibu Tawala,Mkurugenzi na wengine wa kuisaidia Serikalin hakutakuwa na muunganiko wa kuletea wanatarime maendeleo na ofisi isiwe mobile iwe wazi muda wote kusikiliza wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!