Latest Posts

UTORO SHULENI WAIBUA HOJA ZA CAG, RC MALIMA ATOA MAAGIZO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dustan Kyobya, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Ifakara, Pilly Kitwana, kufanya uchunguzi ili kubaini watoto wanaotoroka mashuleni wanakwenda wapi, kwa lengo la kukomesha tabia hiyo.

Maelekezo hayo yametolewa wakati Mkuu huyo wa Mkoa akiongoza kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kilichofanyika katika Halmashauri ya Mji Ifakara.

Malima amesema kuwa utoro wa wanafunzi ni suala nyeti linalohitaji hatua za haraka. Amesema ni muhimu kubaini kata zinazoongoza kwa changamoto hiyo na kushirikiana na waheshimiwa madiwani kuwafuatilia watoto katika maeneo yao ili kuhakikisha utoro unatokomezwa na hoja husika ya CAG inafungwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Dustan Kyobya, amewataka waheshimiwa madiwani kuanza kufuatilia kwa karibu suala la utoro wa wanafunzi katika kata zao kwa kubaini idadi halisi ya watoto walioandikishwa mashuleni na wanaohudhuria masomo. Pia amewasisitiza kuendelea kusimamia amani na utulivu katika maeneo yao.

Naye mwakilishi wa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Stephen Kassaro ameeleza kuwa bado kuna changamoto katika urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Amesema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo kunasababisha ugumu kwa halmashauri kuendelea kutoa mikopo kwa wanufaika wengine.

Sambamba na hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fanya Nakapala amesema kwa niaba ya waheshimiwa madiwani wamepokea maelekezo yote yaliyotolewa na wako tayari kuyatekeleza ili kuhakikisha halmashauri hiyo inaendelea kufanya vizuri katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!