Latest Posts

HATIMA YA MPINA KUJULIKANA SEPTEMBA 11

Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma inatarajiwa kutoa hukumu ya Shauri Namba 21692 la mwaka 2025 kati ya Bodi ya Wadhamini wa chama cha ACT-Wazalendo na Luhaga Joelson Mpina dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali siku ya Alhamisi, tarehe 11 Septemba 2025.

Shauri hilo limesikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu likiongozwa na Mheshimiwa Jaji Abdi Kagomba, ambapo hoja kuu iliyojadiliwa ni uhalali wa hatua ya INEC kumkataa mgombea wa urais kupitia ACT Wazalendo katika mchakato wa uteuzi wa wagombea wa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Katika hati ya madai, upande wa walalamikaji ambao ni ACT Wazalendo kupitia Bodi yake ya Wadhamini pamoja na Luhaga Mpina unadai kuwa mgombea wao alinyimwa haki ya kikatiba ya kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kwa kisingizio kisicho na msingi wa kisheria; hivyo, walalamikaji wameiomba Mahakama itengue uamuzi wa INEC na kutoa amri ya kumtambua mgombea wao kuwa halali kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Kwa upande wao, INEC na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamesimamia uamuzi wao wakisisitiza kuwa taratibu zote za kisheria zilizingatiwa katika mchakato huo, na kwamba mgombea wa ACT Wazalendo hakutimiza masharti ya msingi yaliyowekwa na sheria ya uchaguzi.

Hukumu ya shauri hili inatarajiwa kutolewa rasmi siku ya Alhamisi, tarehe 11 Septemba 2025, katika Mahakama Kuu ya Dodoma kwa njia ya ana kwa ana pamoja na kwa njia ya mtandao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!