Latest Posts

MBIO ZA KOROSHO 2025 KUVUTIA WATOTO, WAZEE NA KUHAMASISHA UTALII WA ZAO LA KOROSHO

Tofauti na mbio nyingine za marathon zinazofanyika nchini, mbio za Korosho Marathon msimu wa mwaka 2025 zinazotarajiwa kufanyika mkoani Mtwara Novemba 29, mwaka huu zimeandaliwa kwa upekee wa kipekee ambapo zitahusisha utalii wa zao la korosho, utalii wa wanyama pamoja na ushiriki wa watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 13.

Akizungumza leo Novemba 10, 2025 wakati wa uzinduzi wa jezi za Korosho Marathon Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema mbio za mwaka huu zitakuwa tofauti na misimu iliyopita kwani kuanzia Novemba 24 hadi 28 kutafanyika maonyesho mbalimbali, yakiwemo maonyesho ya utalii wa zao la korosho, utalii wa wanyama, na mbio maalum za watoto na wazee kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea.

Kanali Sawala ameishukuru Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) pamoja na wadau mbalimbali kwa kuandaa marathon hiyo, akisema tukio hilo litachangia kuongeza thamani ya zao la korosho na kuhamasisha uzalishaji wake ,Aidha amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali kutumia fursa hiyo kujitangaza na kuuza bidhaa zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Korosho Revelian Ngaiza, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo, amesema lengo la kuhusisha makundi ya watoto na wazee ni kuhakikisha makundi yote ya jamii yanapata nafasi ya kushiriki na kutakuwa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la korosho kutoka kwa wajasiriamali wa ndani na nje ya mkoa huo.

Naye Msemaji wa Korosho Marathon Mohamed Kemkem, amesema msimu wa nne wa mbio hizo utakuwa wa kipekee zaidi ukilinganisha na misimu iliyopita, kwani pamoja na mbio, kutakuwa na burudani mbalimbali na maonyesho ya wanyama na amewataka wakazi wa Mtwara na Watanzania kwa ujumla kuendelea kujisajili ili kushiriki kwenye tukio hilo muhimu la michezo, utalii na biashara.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!