Latest Posts

TUNA AMANI YA KUTOSHA, WATANZANIA TUVUMILIANE- KIEDO

Watanzania wamehimizwa kuvumiliana, kudumisha umoja na kuijenga nchi kwa pamoja, wakitakiwa pia kupuuza uvumi mbalimbali unaoelezwa kwenye Mitandao ya Kijamii kwamba  Askari Polisi na Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamekuwa wakikamata na kupiga wananchi wasiokuwa na hatia ama makosa ya kisheria.

Wito huo umetolewa na Mzee Mbarak Hassan Kiedo (75) wakati alipozungumza nasi kuhusiana na hali ya usalama na amani katika eneo lake la Temeke Mkoani Dar Es Salaam, mara baada ya vurugu na uharibifu wa wachache uliofanywa Oktoba 29, 2025 kwa makundi ya watu kuiba, kuharibu na kuteketeza kwa moto mali za umma na za watu binafsi.

“Sisi tupo shwari, tunaishi kwa amani na umetukuta hapa Chanika tukiwa hatuna hata ngeu (majeraha ya kupigwa). Serikali haina ugomvi na raia wake hata kidogo na sisi tunawajibika kutii na kusikiliza kile tunachoelekezwa kufanya.” Amesema Mzee Kiedo.

Amezungumzia pia jitihada zilizochukuliwa na serikali na Vikosi vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha raia wake wanasalia salama, akisema zuio la kutotoka nje kuanzia saa kumi na mbili jioni pamoja na maelekezo mengine yaliyokuwa yametolewa Oktoba 29, 2025 na siku zilizofuata ilikuwa ni katika kuhakikisha jamii inabaki salama na uhalifu na wahalifu wanadhibitiwa kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Amerejea msimamo wake wa kubainisha kuwa nchi ni salama na tulivu na zaidi Mkoa wa Dar Es Salaam, akisema walikuwa wachache pekee waliotubuniwa kwa tamaa zao na kuamua kufanya uhalifu na uharibifu, akifananisha na Mechi za Simba na Yanga, pale mmoja anaposhindwa na kuamua kuleta vurugu isiyokuwa na sababu za msingi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!