Latest Posts

MSANII PENGO KUCHOCHEA UTALII WA NDANI

Msanii wa vichekesho, Fadhiri Atiki maarufu kama Pengo Makeke, ametangaza rasmi kuanza kwa ziara yake ijulikanayo kama Pengo Makeke Mbeya Tour, yenye lengo la kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana mkoani Mbeya.

Akizungumza katika mkutano huo, Pengo Makeke amesema kuwa Mbeya ni mkoa wenye hazina kubwa ya vivutio vya asili, historia na utamaduni ambavyo bado havijatangazwa vya kutosha ndani na nje ya nchi.

Amesema kupitia sanaa yake, anataka kuchochea mwamko wa utalii wa ndani na kuwafanya Watanzania na wageni wavifahamu zaidi vivutio hivyo.

Kwa upande wake, Godwin Mwambaja, muongoza watalii kutoka Chikanda Safari, amesema watahakikisha wanashirikiana kikamilifu katika kuutangaza utalii wa Mbeya ili wageni wanapowasili wajue maeneo mengi mazuri yaliyopo mkoani humo.

Naye Afisa Utalii kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services Agency (TFS)) – Nyanda za Juu Kusini, Jesca Mgata, amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara na huduma muhimu ili kurahisisha upatikanaji wa vivutio hivyo kwa watalii.

Ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuwekeza katika vivutio hivyo ili kuongeza thamani na kuvutia wageni wengi zaidi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!