Latest Posts

RAIS SAMIA: ZANZIBAR IMEVUKA WATALII MILIONI 1, ONGEZEKO LA ZAIDI YA ASILIMIA 20 KITAIFA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema sekta ya utalii nchini inaendelea kukua kwa kasi kubwa.

Akizungumza leo katika kilele cha Maonesho ya Sanaa za Picha yaliyofanyika Kizimkazi, Zanzibar, Rais Samia amebainisha kuwa Zanzibar pekee imepokea watalii zaidi ya milioni 1.0 hadi mwaka jana 2025.

Kwa mujibu wa Rais Samia, idadi hiyo ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka 2024 ambapo Zanzibar ilipokea watalii laki 7 tu sawa na asilimia 20.4 ya watalii wanaingia kila mwaka, jambo linaloonesha dhamira ya serikali katika kuitangaza Tanzania kimataifa.

Rais Samia amewataka wadau wa sekta ya utalii kutokobweteka na takwimu hizo za mafanikio. Amesisitiza kuwa sasa ni wakati wa kuongeza mnyororo wa thamani katika shughuli za utalii ili wananchi, hususan vijana, wanufaike moja kwa moja. “Tusisimame kwenye namba tu, tuhakikishe kila mtalii anakuja anaacha fedha katika mikono ya Mtanzania,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais amewapongeza na kuwataka vijana wabunifu kuendelea kupiga picha nzuri zinazotangaza vivutio vya nchi. Amesema serikali itaendelea kuwatengenezea mazingira wezeshi ikiwemo masoko ya kimataifa ili kazi zao ziweze kuuzwa na hatimaye kuongeza kipato kwao na kwa Taifa kwa ujumla.

Hatimaye, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewashukuru wadau wote waliofanikisha maonesho hayo. Amesema maonesho hayo ni ushuhuda tosha wa namna vijana wa Kitanzania wanavyoweza kupiga picha za kuvutia kitalii, jambo ambalo linaipa nchi sura nzuri na kuitangaza hadi ngazi ya kimataifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!