Latest Posts

ACT YATEUA JINA LA ANAYEPENDEKEZWA KUWA MAKAMU WA RAIS WA ZANZIBAR

Chama cha ACT Wazalendo kimesema kimefanya uteuzi wa jina la mwanachama anayependekezwa kushika nafasi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chama hicho leo Septemba 17, 2026 iliyotolewa chini ya Katibu Mkuu wake Ado Shaibu, imesema Chama hicho kiliteua jina hilo Jana Septemba 16, 2026 chini ya ibara ya 72(3)(f) ya Katiba ya Chama.

Taarifa hiyo imesema kuwa jina hilo litawasilishwa rasmi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa ajili ya kukamilisha utaratibu uliowekwa na Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 39(1), (2) na (3).

Kikao hicho maalumu cha Kamati ya Uongozi Taifa kilifanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Zanzibar, Vuga mjini Unguja.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!