Latest Posts

WANANCHI WA KILAMBO WAONYWA KUTOPUUZA HATARI YA MAFURIKO

Wananchi wanaoishi katika maeneo ya jirani na Mto Ruvuma, Kijiji cha Kilambo, Kata ya Tangazo, wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya uwezekano wa mafuriko yanayoweza kusababishwa na mvua za El-Nino, ambazo zinaweza kuharibu mashamba, kuvamia makazi na kuhatarisha maisha ya watu.

Mkurugenzi wa Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini, Sudi Mpemba, amesema Mto Ruvuma hupokea maji kutoka nchi jirani za Msumbiji na Malawi, hali inayoweza kusababisha kuongezeka kwa maji na kuleta athari kwa wananchi wanaoishi maeneo ya kandokando ya mto huo.

Meneja wa Mazingira na Mratibu wa Jumuiya za Watumia Maji wa Bodi ya Maji, Bonde la Ruvuma na Pwani ya Kusini, Batuli Mwarondo, amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa mamlaka husika, hususan Bodi ya Maji, wanapoona viashiria vya hatari ili kuwezesha hatua stahiki kuchukuliwa.

Kwa upande wake, Mhaidrolojia Mwandamizi wa bonde hilo, Jaribu Modest, amesema Mto Ruvuma wenye urefu wa takribani kilomita 800 unapofika eneo la Mto Mtwara huwa na kina kifupi na eneo pana, hali inayoweza kusababisha maji kutawanyika hadi katika upana wa takribani mita 500 na kuathiri makazi ya wananchi.

Nao baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kilambo, akiwemo Ally Mponda, wamewataka wananchi wenzao kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Serikali na kuacha kuchukulia mafuriko kama jambo la kawaida, wakisisitiza umuhimu wa kuchukua tahadhari ili kulinda maisha na mali zao.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!