
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), tarehe 21 Oktoba 2026, amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na makundi mbalimbali katika Kata ya Buigiri, Kijiji cha Buigiri, Jimbo la Chamwino, kujitokeza kwa wingi Novemba 4, 2026, kumpigia kura Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Chamwino kupitia CCM, Dkt. Netho Ndilito, ili kuonesha nguvu ya Chama Cha Mapinduzi.
Chatanda ameyasema hayo katika mkutano wa ndani uliofanyika katika Kata ya Buigiri, Kijiji cha Buigiri, ambapo amewataka wanachama na makundi mbalimbali kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi na kumuunga mkono mgombea wake ili kuendeleza juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo katika Jimbo la Chamwino.