
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC), tarehe 21 Oktoba 2026, amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa Jimbo la Chamwino kujitokeza kwa wingi tarehe 4 Novemba 2026 kumpigia kura Dkt. Netho Ndilito*, mgombea wa Ubunge kupitia CCM, ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Deogratius Ndejembi baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Chatanda ametoa wito huo katika Mkutano wa Ndani uliofanyika katika Kata ya Chamwino, Kijiji cha Chamwino, Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma, ambapo ameeleza kuwa baadhi ya vikundi vinapita kuwaomba wananchi kura, ilhali havina Serikali ya kutekeleza na kusimamia mipango ya maendeleo katika jimbo hilo.
Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutambua umuhimu wa kumchagua mgombea wa CCM, akieleza kuwa chama hicho ndicho kinachoongoza Serikali na kina uwezo wa kuendelea kusimamia utekelezaji wa mipango na miradi ya maendeleo katika Jimbo la Chamwino.