Latest Posts

MAKAMU WA RAIS AKERWA NA UDANGANYIFU TANROADS MBEYA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekerwa na uzembe na taarifa za kupotosha kuhusu ufunguaji wa barabara ya njia nne mkoani Mbeya, kuwapunguzia adha watumiaji wa barabara hiyo, baada ya kurejea kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika eneo la Kabwe.

Makamu wa Rais amechukizwa na kitendo cha Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Suleiman Bishanga, kutoa maelezo ya kupotosha kuhusu kuanza kufungua barabara katika eneo la Mdope mkoani humo. Akionesha kutoridhishwa na hali hiyo, Makamu wa Rais amehoji namna Serikali inavyotoa fedha nyingi bila kuona matokeo yanayolingana na thamani yake, akisisitiza kuwa shilingi bilioni 40 si fedha ndogo kiasi cha kuruhusu uzembe na usimamizi dhaifu.

Makamu wa Rais amemtaka Waziri wa Ujenzi, Mhe. Masanja Kadogosa, kuhakikisha hatua za uwajibikaji zinachukuliwa kuanzia kwa Meneja wa TANROADS aliyempatia taarifa zisizo sahihi, akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia watendaji wanaowadanganya viongozi huku wananchi wakiendelea kupata adha ya miundombinu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!