Latest Posts

VIONGOZI WA DINI, WAZEE WANA NAFASI KUBWA KULINDA JAMII – RC SENDIGA

 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Queen Cuthbert Sendiga, amesema kuna umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya wazee, watu maarufu, viongozi wa dini na Serikali katika kubaini maeneo yenye changamoto za tabia zisizofaa, ili kuchukua hatua stahiki za kukomesha vitendo vya ukatili, kulinda maadili na kujenga jamii salama kwa wote.

Sendiga ameyasema hayo Oktoba 8.2026, wakati akizungumza katika kikao na viongozi wa dini na wazee wa Mkoa wa Morogoro kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Aidha, amewataka viongozi wa dini, wazee pamoja na watu maarufu kutumia nafasi na ushawishi walionao kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazotarajiwa kunyesha, hususan kuwaelimisha waumini na jamii kuondoka katika maeneo hatarishi yaliyo karibu na vyanzo vya maji.

Vilevile, amewataka viongozi hao kuendelea kuhamasisha wananchi kufanya usafi katika maeneo yao, ikiwemo kusafisha mitaro na njia za maji, ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi na kuzuia maji kutuama kwa muda mrefu.

Sendiga amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanakuwa salama, maadili yanaendelea kulindwa na changamoto zinazoweza kuhatarisha ustawi wa jamii zinadhibitiwa kwa wakati.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!