Latest Posts

SENDIGA AAGIZA WATUMISHI KUPIMA AFYA KILA MIEZI MITATU

 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Best Magoma, kuhakikisha watumishi wa umma wanapima afya zao kwa hiari kila baada ya miezi mitatu ili kubaini mapema magonjwa na kuchukua hatua stahiki.

Sendiga ametoa maelekezo hayo leo, Oktoba 28, 2026, wakati akizindua Wiki ya Maadhimisho ya Lishe ngazi ya mkoa, iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakikosa utaratibu wa kupima afya zao kutokana na majukumu ya kikazi, huku akiwahimiza kujenga utamaduni huo ili kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, yakiwemo shinikizo la damu na kisukari.

Kwa upande wake, Afisa Lishe wa Mkoa wa Morogoro, Salome Magembe, amesema jumla ya watu 309 wamepimwa afya zao tangu zoezi hilo lianze, wakiwemo watumishi 109. Huduma zinazotolewa ni pamoja na upimaji wa hali ya lishe, shinikizo la damu, sukari na uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake pamoja na tezi dume kwa wanaume.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!