Latest Posts

RAIS AMTEUA ANGELINE MABULA KUWA RC TABORA, MALISA ATENGULIWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Umma, ikiwa ni pamoja na kumteua Bi. Angeline Lubala Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, pamoja na kuwateua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wapya wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo, Oktoba 28, 2026, na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Shaaban Kissu, kufuatia taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

Rais Samia amemteua Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza Bi. Angeline Mabula kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, akichukua nafasi ya Bw. Beno Morris Malisa ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Vilevile, Rais Samia amefanya uteuzi wa viongozi wakuu wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kumteua Bw. Dunford George Mpelumbe kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mpelumbe alikuwa Wakili wa Serikali katika Ofisi ya

MALISA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bw. Mpelumbe anachukua nafasi ya Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mwaimu ambaye amemaliza muda wake wa utumishi.

Pia, Rais amemteua Bw. Omar Ali Omar kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Omar alikuwa Mkuu wa Idara ya Utawala, Mipango na Fedha katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Zanzibar, ambapo anachukua nafasi ya Bw. Mohamed Khamis Hamad ambaye naye amemaliza muda wake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!