Latest Posts

NBS: AI, BIG DATA KUIBUA FURSA MPYA KWA WATAALAM WA TAKWIMU.

Wataalamu wa takwimu nchini wamehimizwa kutumia majukwaa ya mtandaoni kujifunza teknolojia mpya ikiwemo Akili Unde (AI), Big Data na Data Science ili kuongeza ushindani wao katika soko la ajira kuelekea mwaka 2030.

‎Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu, Utafiti na Shughuli za Kitakwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), James Mbongo, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Saba wa Chama cha Wataalamu wa Takwimu Tanzania (TASTA) uliofanyika jijini Dodoma.

‎Mbongo amesema mabadiliko ya teknolojia yamebadili namna taarifa zinavyokusanywa na kuchambuliwa, hivyo wataalamu wa takwimu wanahitaji kuongeza maarifa ili kuendana na mabadiliko hayo na kutoa taarifa zenye ubora na usahihi.

‎Amesema takwimu ni msingi muhimu wa maamuzi yanayofanywa na Serikali pamoja na sekta binafsi, kuanzia katika kupanga mipango ya maendeleo, kusimamia utekelezaji wake hadi kutathmini mafanikio yaliyopatikana.

‎

‎

‎Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TASTA, Abdallah Mhagama, amesema chama hicho kinaunganisha wataalamu kutoka taasisi za Serikali na sekta binafsi ili kuimarisha ushirikiano na ubora wa takwimu nchini.

‎Naye Makamu Mwenyekiti wa TASTA, Mariamu Kinabo, amesema changamoto ya fedha imekuwa kikwazo katika kuwakutanisha wanachama waliopo katika mikoa na wilaya mbalimbali.

‎Amesema gharama za usafiri, malazi, chakula na maandalizi ya mikutano zimeathiri utekelezaji wa mpango wa kukutana mara kadhaa kwa mwaka, ambapo kwa sasa mikutano hiyo hufanyika kwa wastani wa mara moja kwa mwaka.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!