Latest Posts

MANISPAA YA GEITA WAANZA UJENZI WA UWANJA WA MAGOGO KWA KUTUMIA WATAALAMU WA NDANI

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Geita, Leonard Kiganga Bugomola, amesema Manispaa hiyo imeanza mchakato wa ujenzi wa Uwanja wa Magogo kwa kutumia wahandisi wake wa ndani, hatua inayolenga kupunguza gharama za ujenzi na kubana matumizi ya fedha za umma.

Bugomola amesema hayo leo, Novemba 10, 2026, wakati wa mkutano wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2026/2027, uliojadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Manispaa hiyo, yakiwemo changamoto zinazozikabili kata pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Geita, lililolenga kuhakikisha wataalamu na watumishi wa Serikali wenye uwezo wa kutekeleza shughuli za ujenzi wanatumika ipasavyo, badala ya kuajiri wakandarasi kutoka nje, ili kupunguza gharama na kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma.

Ameongeza kuwa wameona ni vyema kuanza kutekeleza agizo hilo kupitia mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Magogo kwa kutumia wahandisi na mafundi wa Manispaa hiyo, hatua itakayosaidia kupunguza gharama za utekelezaji wa mradi huo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Yefred Muyenze, amesema lengo ni kuhakikisha uwanja huo unakamilika ifikapo Februari 6, huku akieleza kuwa mafundi tayari wanaendelea na kazi za ujenzi ili kukamilisha mradi huo ndani ya muda uliopangwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!