Latest Posts

HALIDI ANASWA TUHUMA ZA KUBOMOA, KUHARIBU MALI ZA MWAJIRI WAKE

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia na kumhoji kwa kina Halidi Seleman Kalaghe (45), mwendesha mtambo aina ya ‘Excavator’, kwa tuhuma za kuharibu mali mbalimbali za mwajiri wake kufuatia mzozo uliotokea kati yao.

Hatua hiyo imebainishwa katika taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa leo, Novemba 11, 2026, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Polisi, tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 10 Novemba, 2026, majira ya saa 06:05 mchana katika Mtaa wa Mvumoni, Somangila, uliopo ndani ya Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alifikia uamuzi wa kufanya uharibifu huo katika mazingira yaliyozua taharuki kubwa baada ya kutokea kwa kutoelewana kati yake na mwajiri wake, kampuni ya China Energy Engineering Group Guanxi Hydroelectric Construction Bureau CO.LTD, inayotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara katika Manispaa hiyo ya Kigamboni.

Baada ya kutoelewana huko, Kalaghe anadaiwa kuingia kwenye mtambo wa ‘Excavator’ na kuanza kubomoa na kuharibu mageti mawili pamoja na uzio wake, gari ndogo yenye namba za usajili T 282 DEM aina ya Toyota Sienta mali ya Brighton Abraham Mfangavo, gari la kubebea mafuta namba T 391 EUN aina ya Sinortrack mali ya kampuni hiyo, pamoja na nyumba za muda zenye vyumba vitano na vyoo.

“Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam imemkamata Halidi Seleman Kalaghe, miaka 45, Mwendesha mtambo ‘Excavator’ kwa tuhuma za kuharibu mali za mwajiri wake. Tukio hilo limetokea tarehe 10 Novemba, 2026 saa 06:05 mchana Mtaa wa Mvumoni Somangila Kigamboni Dar es Salaam katika mazingira yaliyozua taharuki baada ya kutoelewana na mwajiri wake kampuni ya China Energy Engineering Group Guanxi Hydroelectric Construction Bureau CO.LTD inayofanya kazi za ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Kigamboni alichukua uamuzi wa kuingia kwenye mtambo ‘Excavator’ na kuanza kuharibu mageti mawili na uzio wake, gari ndogo yenye namba T 282 DEM aina ya Toyota Sienta mali ya Brighton Abraham Mfangavo, gari la kubebea mafuta namba T 391 EUN aina ya Sinortrack mali ya kampuni, nyumba za muda zenye vyumba vitano na vyoo”, ameeleza Muliro.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa taratibu zaidi za kisheria zinaendelea kukamilishwa dhidi ya mtuhumiwa huyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!