Latest Posts

SEMU: KESI YA TUNDU LISSU INAHITAJI SULUHISHO LA KISIASA NA SIO VINGINEVYO

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ametoa wito wa kuachiliwa huru kwa kiongozi wa kisiasa Tundu Lissu, akieleza kuwa kesi inayomkabili ni ya kisiasa na inahitaji suluhisho la kisiasa.

Amebainisha hayo Novemba 4, 2026 alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Kata ya Nyarubanda, Jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma.

“Kesi ya Tundu Antipas Lissu ni kesi ya kisiasa na inahitaji suluhisho la kisiasa na siyo vinginevyo. Iwe iwavyo, sisi tunajua demokrasia itaendelea kupiganiwa,” amesema Semu.

Aidha, kuhusu matukio ya Oktoba 29 na siku zilizofuata, Semu amebainisha kuwa umepita mwaka mmoja bila kiongozi yeyote kuwajibika, huku Serikali ikiunda tume mbalimbali ambazo amedai kuwa ni za kujificha kwenye ukweli. Amesisitiza haja ya kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi ya kimataifa isiyoegemea upande wowote ili kuweka wazi ukweli wa kilichotokea, kuwapa haki waliopoteza maisha na majeruhi, na kuwawajibisha waliohusika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!