Latest Posts

WASIRA AUNGA MKONO MSIMAMO WA LEMA KUHUSU WANAHARAKATI

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amewataka wanasiasa na wanaharakati nchini kuendesha mijadala ya kisiasa kwa kutumia hoja zenye tija badala ya kutegemea matusi na uchochezi, akisisitiza kuwa CCM haina uhasama na chama chochote cha upinzani nchini.

Wasira aliyasema hayo leo, Novemba 3, 2026, wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa kufunga kampeni za mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma. Ameeleza kuwa chama hicho tawala hakikatai kukosolewa, bali kinakaribisha ukosoaji wenye kujenga unaolenga kuonesha mapungufu ili yafanyiwe kazi, badala ya kutumia mitandao ya kijamii kutoa lugha za matusi dhidi ya viongozi.

Katika hotuba yake, Wasira amegusia suala la wanaharakati na kueleza kuwa amekubaliana na baadhi ya hoja zilizowahi kutolewa na mwanasiasa wa CHADEMA, Godbless Lema kuhusu uwepo wa baadhi ya wanaharakati walioko nje ya nchi. Amebainisha kuwa mnamo Januari 25, 2025, baadhi ya wanaharakati hao walishiriki katika uchaguzi wa CHADEMA kwa lengo la kumwondoa Freeman Mbowe na kumweka Tundu Lissu.

Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa maelezo ya Lema, baada ya kufanikisha mabadiliko hayo, wanaharakati hao walianza kuingilia uendeshaji wa chama hicho kwa kutoa maelekezo, amri, na wakati mwingine kuvuka mipaka kwa kutoa matusi dhidi ya viongozi wa CHADEMA bila sababu za msingi.

“Tunataka wanaharakati wa hoja, si wanaharakati wa kutukana. Wanatusaidia pale wanapotuambia mmefanya makosa haya na haya, sisi hatukatai kukosolewa,” amesisitiza Wasira, akiongeza kuwa hata kama mtu ni mpinzani au mpinzani wa kisiasa, anapozungumza jambo la kweli anapaswa kusikilizwa.

 

Msimamo wa CCM na Masuala ya Kisheria

Kuhusu uhusiano wa CCM na vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, Wasira alisisitiza kuwa chama chake hakina ugomvi nao, lakini kinataka shughuli za kisiasa zifanyike kwa kuzingatia sheria na misingi ya ustaarabu.

Aidha, akizungumzia baadhi ya hoja zilizowahi kutolewa katika mazungumzo ya kisiasa, Wasira alibainisha kuwa suala la Tundu Lissu liko mikononi mwa vyombo vya sheria (Mahakama), hivyo Serikali haiwezi kuingilia mwenendo wake, sambamba na kupinga pendekezo la kuhusisha mpatanishi kutoka nje ya nchi katika masuala ya ndani ya nchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!