Latest Posts

ACT YAMSHAURI RAIS SAMIA MAMBO MATATU KUFIKIA ‘MARIDHIANO YA KWELI’

Chama cha ACT Wazalendo kimetoa ushauri wa mambo matatu makuu kwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ili kufikia maridhiano ya kweli na ya kudumu nchini, kikisisitiza kuwa nchi haiwezi kuwa na utulivu bila misingi ya ukweli, haki na uwajibikaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Uhusiano kwa Umma wa ACT Wazalendo, Shangwe Ayo, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu ameeleza hayo Agosti 1, 2026, jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Madiwani wa chama hicho kutoka kata mbalimbali nchini.

Semu ameeleza kuwa ili mchakato wa maridhiano uwe na tija na maana kwa wananchi, Serikali inapaswa kuwaachia huru wafungwa wote wa kisiasa nchini, kuruhusu uchunguzi huru wa kimataifa kuhusu matukio ya mauaji yaliyotokea tarehe 29 Oktoba 2025 na kutoa ramani ya wazi ya kupatikana kwa Katiba Mpya ya wananchi na kuanza mchakato wa kupatikana kwake.

Semu amebainisha kuwa mambo hayo matatu tayari yameshawasilishwa rasmi kwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wake na viongozi wa vyama vya siasa, na kwamba msimamo huo uliridhiwa na Kamati Kuu ya chama hicho katika vikao vyake vya Januari na Aprili 2026.

“Sisi tumetekeleza wajibu wetu wa kuyawasilisha. Wajibu wa Rais Samia na Serikali yake ni kuyatekeleza. Tutaendelea kusimama imara iwapo hatutaona nia ya dhati ya kuyatekeleza,” alisema Semu.

Katika hatua nyingine, Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo amewataka madiwani wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kutetea msimamo huo wa uwajibikaji, huku wakiweka maslahi ya wananchi mbele. Aliwaagiza kusimamia kwa umakini matumizi ya rasilimali za umma na kulinda haki za wananchi katika kata wanazoziongoza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!