Latest Posts

CHADEMA YAJIBU TUHUMA DHIDI YA HECHE: “WANALIPWA MILIONI MBILI KUCHAFUA VIONGOZI”

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika amesema kama kuna mwanachama yeyote wa chama hicho ambaye ana taarifa zozote za malalamiko anapaswa kufuata taratibu za kikatiba za chama hicho.

Mnyika amesema hayo leo Julai 10, 2026 akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho Mikocheni mkoani Dar es Salaam na kueleza kuwa walikuwa na taarifa kuwa wale ambao wamekuwa wakitoa tuhuma dhidi ya viongozi wamekuwa wakilipwa fedha mpaka milioni mbili kwa lengo la kuchafua viongozi.

“Kuna taarifa tulikuwepo nazo uwepo wa watu wanaoshawishi viongozi kufanya hizo press kwa kupewa pesa kwamba mtu anapewa milioni mbili… kuna usaliti na kutumika kutaka kukichafua chama na viongozi wake kama mtu ana malalamiko dhidi ya yoyote kwenye jambo lolote afuate utaratibu wa kikanuni na kikatiba”, amesema Mnyika.

Maelezo hayo ya Mnyika ameyatoa kutokana na kuwepo kwa taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho (kupitia vyombo vya habari) wakidai uwepo wa rushwa na ufisadi unaofanywa na Makamu Mwenyekiti.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!