Latest Posts

HECHE ASHANGAZWA KULINGANISHWA NA WASIRA, ASISITIZA MAMBO MAWILI

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amekosoa vikali taratibu za uchaguzi na demokrasia ya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akidai kuwa chama hicho kilivunja kanuni zake wenyewe wakati wa kupitisha viongozi na mgombea wake wa Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza leo, Septemba 24, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Heche ameeleza kuwa CHADEMA iliweka msimamo wa kutoshiriki katika mchakato ambao hata ndani ya CCM yenyewe kanuni zake zilikiukwa

Heche amebainisha kuwa katika kikao cha mkutano mkuu wa chama hicho, ajenda ilibadilishwa ghafla bila kufuata taratibu za kuchukua fomu, kujaza fomu, wala kusaka wadhamini, na badala yake viongozi walipitishwa kwa kuinua tu mikono

“Wanataka kumpitisha Wasira kama Makamu Mwenyekiti kama mimi, eti Wasira naye wanamlinganisha na mimi, ndugu zangu hebu oneni hizi dharau wanazotuletea hawa jamaa. Sasa ajenda ya mkutano mkuu ilikuwa ni tofauti… Wakaigeuza, mtu akanyanyua mkono akasema mimi naomba tumpitishe Rais moja kwa moja”.

Hata hivyo, viongozi wakuu wa chama hicho akiwamo aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla walijibu kuwa chama hicho hakikubadili gia angani kwa kuwateua wagombea urais mapema kuelekea uchaguzi wa mwaka huo kwani uamuzi uteuzi wao ulichochewa na shinikizo la wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, baada ya kuridhishwa na namna makada hao walivyotekeleza ilani.

Akisisitiza msimamo na madai makuu ya CHADEMA mbele ya wananchi wa Bariadi, Heche amebainisha kuwa chama hicho kina mambo mawili makuu kinachoyapigania kwa sasa, ikiwemo kutaka Mwenyekiti wake wa chama taifa, Tundu Lissu kuachiwa huru.

“Sisi CHADEMA tukasema hatuwezi kwenda kwenye huo uchaguzi ambao hata kuanzia ndani ya CCM yenyewe kanuni zao zimevunjwa… Ndio maana tunakuja kwenu sasa tunasema mambo mambo yetu ni mangapi? Mawili. Moja, tunataka mwenyekiti wetu aachiwe awe huru kwa sababu hana kosa kwa kudai katiba. Jambo la pili, tunataka Katiba Mpya”, ameeleza Heche.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!