Latest Posts

MUME ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKE WAKE KWA JEMBE

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limemkamata na linaendelea kumhoji Emmanuel Evance Simon (52), mkazi wa Kijiji cha Chisegu, Kata ya Chanikanguo, Wilaya ya Masasi, kwa tuhuma za kumuua mke wake, Clauda Yohana Bakari (54).

Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 10 Novemba, 2026 majira ya saa nane mchana huko maeneo ya Chanikanguo, ambapo mtuhumiwa anadaiwa kumjeruhi mke wake kwa kumkata na jembe maeneo ya kisogoni na kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo chake

Taarifa rasmi iliyotolewa Novemba 11, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleimani imeeleza kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi, baada ya mtuhumiwa kumtuhumu marehemu mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.

Jeshi la Polisi limebainisha kuwa uchunguzi wa shauri hilo unaendelea na pindi utakapokamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani

“Mtuhumiwa alitenda kosa hilo mnamo tarehe 10 Novemba 2026 majira ya saa nane mchana… Chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi,” imeeleza taarifa hiyo.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limetoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi wanapokabiliwa na migogoro ya kimaisha, na badala yake watumie njia sahihi na za kisheria kusuluhisha changamoto zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!