Latest Posts

DC SAME ARIDHISHWA NA UJENZI WA JENGO LA TAALUMA CHUO CHA UUGUZI

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni,ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la Taaluma katika Chuo cha Uuguzi na Ukunga Same, ambao umefikia asilimia 64 na kuwa mbele ya muda uliopangwa kwa siku 14 ambapo kukamilika kwake utakuwa na uwezo wa kupokea wanafunzi 600 kwa wakati mmoja.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo Novemba 10,2026 akiwa na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Mgeni amesema kukamilika kwa jengo hilo kutaimarisha mazingira ya mafunzo na kuongeza uwezo wa chuo kutoa wataalamu wa uuguzi na ukunga watakaosaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Amemtaka mkandarasi kuhakikisha anakuwepo eneo la kazi wakati wote ili kusimamia ubora wa ujenzi, kuhifadhi nyaraka za mradi na kudhibiti upotevu au wizi wa vifaa, akieleza kuwa usimamizi madhubuti ni muhimu katika kuhakikisha fedha za Serikali zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha za mradi huu, unaotarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mafunzo ya wataalamu wa afya na huduma zinazotolewa kwa jamii”alisema DC Mgeni.

Kwa upande wake, Mhandisi wa mradi Msanifu Kassim, amesema ujenzi umefikia asilimia 64 na uko mbele ya mpango kwa siku 14, akiahidi kuhakikisha kazi inakamilika kwa wakati uliopangwa.

Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni tano unafadhiliwa na Serikali kupitia mkopo wa Benki ya Dunia chini ya Programu ya Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto Tanzania (TMCHIP). Ulianza Aprili 1, 2026 na unatarajiwa kukamilika Mei 2027.

Jengo hilo litakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa wakati mmoja, jambo litakaloongeza fursa za mafunzo ya wataalamu wa afya na kuchangia upatikanaji wa huduma bora za uuguzi na ukunga kwa wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!