Latest Posts

MARANJE KUWA KITOVU CHA UCHAKATAJI WA KOROSHO TANZANIA

Tanzania inatarajia kuongeza uwezo wa kuchakata korosho ndani ya nchi kupitia ujenzi wa Kongani la Viwanda katika Kijiji cha Maranje, Halmashauri ya Nanyamba mkoani Mtwara, mradi unaolenga kujenga miundombinu ya kisasa ya viwanda vya kubangua na kuongeza thamani ya zao hilo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kongani hiyo Novemba 13, 2026, katika ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara.

 

Mradi huo unaosimamiwa na Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), unatarajiwa kuongeza shughuli za uchakataji wa korosho nchini na kufungua fursa za ajira kwa wananchi wa Mtwara na maeneo jirani.

Katika hafla hiyo, Ndejembi ameelekeza bomba la gesi kufikishwa katika eneo la kongani na kuiagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuweka miundombinu ya umeme kwa ajili ya kuhakikisha viwanda vitakavyokuwepo vinapata nishati ya kuendesha shughuli zake.

Aidha, amekabidhi mashine 100 za kisasa za kubangua korosho kwa wabanguaji wadogo, kila moja ikiwa na uwezo wa kubangua kilo 700 kwa siku, hivyo mashine zote kuwa na uwezo wa kuchakata jumla ya kilo 70,000 kwa siku.

Mashine hizo zinatarajiwa kuchangia upanuzi wa shughuli za ubanguaji na kutoa fursa za ajira zaidi ya 4,000, hususan kwa vijana wa mkoa wa Mtwara.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!