Latest Posts

VETA YAAZIMIA KUONDOKA NA USHINDI SHIMMUTA

Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kwa wanaume na timu ya mpira wa pete kwa wanawke za VETA zinazoshiriki kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Kampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) wamehimizwa kuendelea kucheza kwa bidi na kutafuta ushindi ili kuendelea na hatua zinazofuata na hatimaye kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

‎Akizungumza na wachezaji hao Mkurugenzi wa Fedha kutoka VETA Makao CPA. Fedilis Tungu, kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu, katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Uwalimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC), leo tarehe 12 Novemba, 2026 amesema timu hizo mbili zinazoshiriki mashindano hayo hazina budi kuendelea kupambana kwa hali namali ilikupata ushindi mnono , kusonga katika hatua nyingine hatiamaye kutwaa ubingwa.

‎Sambamba na hilo ameipongeza timu ya mpira wa pete ya wanawake kwa kufanikiwa kuingia 32 Bora katika mashindano hayo, timu hiyo ilikuwa kundi D lenye jumla ya timu tano ambazo ni ATCL, TRA, MOI, BRELA na VETA yenyewe, timu hiyo imeshika nafasi ya 3 katika kundi lake na kufanikiwa kuvuka hatua hii ya makundi kwa mara ya kwanza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!