Latest Posts

BALOZI WA UINGEREZA, DC ARUMERU WAJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Marianne Young, amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya wilaya hiyo na serikali ya Uingereza katika kuvutia uwekezaji na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara.‎

‎Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, viongozi hao wamejadili fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo wilayani humo pamoja na umuhimu wa kuweka mazingira wezeshi yatakayovutia wawekezaji wapya kutoka Uingereza na kuwawezesha wale waliopo kuendeleza shughuli zao.

‎

‎Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Neema Lugangira, amekubaliana na Balozi Marianne Young kuwa baada ya kukamilisha ziara yake ya Kata kwa Kata wilayani humo, atawasilisha vipaumbele vya maendeleo ya wilaya ili kubainisha maeneo mahsusi ya ushirikiano kati ya ofisi yake na Ubalozi wa Uingereza.

‎Hatua hiyo inalenga kuweka msingi wa ushirikiano katika kutambua fursa za uwekezaji na kuhamasisha utekelezaji wa miradi itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Arumeru.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!