Latest Posts

RC MALIMA: TUMIENI MASHINDANO YA GOFU KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima amewataka waandaaji wa mashindano ya gofu ya Alliance one Morogoro Open yanayotarajiwa kufanyika kuanzia Juni 14 hadi 16 mwaka huu kutumia mashindano hayo kutangaza vivutio vya utalii ambavyo vipo ndani ya mkoa huo.

Ameyasema hayo Jumamosi Juni 8, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani  hapo ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa kutumia michezo katika kutangaza vivutio hivyo ili kuweza kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii.

Katibu wa Chama cha Gofu Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya Morogoro Gymkhana Dickson Sika amesema zaidi ya wachezaji 80 wa mchezo wa gofu kutoka mataifa matatu wanatarajia kushiriki mashindano ya Alliance one Morogoro Open huku mwitikio wa wachezaji kwa mwaka huu ukiwa ni mkubwa na amewataka wananchi kujitokeza kushiriki mashindano hayo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!