Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro leo Mei 4, 2024 ameongoza hamasa ya kucheza mchezo wa Gofu kwa madiwani wa Manispaaa ya Morogoro kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya mchezo huo huku akitoa wito kwa jamii kushiriki kucheza mchezo huo.
Akizungumza wakati wa hamasa hiyo mkoani Morogoro Dkt.Ndumbaro amesema kuwa ni wajibu wa kila mwana Morogoro kutunza miundombinu ya michezo ukiwemo uwanja Gofu Gymkhana uliopo mkoani humo
“Wito wangu kwa Watanzania wote tupende michezo na mchezo wa gofu ni mmoja kati ya michezo ambayo haichagui umri mtu yeyote anaweza kucheza” Ameseama Dkt. Ndumbaro
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima ameitaka jamii kuacha dhana ya kufikiri kuwa mchezo wa Gofu ni wa watu wenye kipato cha juu badala yake wajifunze mchezo huo kwa kuwa una manufaa makubwa.