Latest Posts

FAHAMU KUHUSU JARIBIO LA TRUMP KUUAWA, NA KAMPENI ZAKE ZA URAIS MAREKANI

Si rahisi kutokea lakini ndio imeshakuwa.

Naam ni shambulizi la mgombea urais hasa katika taifa lenye nguvu na ulinzi wa hali ya juu kama Marekani, japokuwa vimeshatokea vifo kadhaa vya marais na watu wakubwa wa taifa hilo kwa kushambuliwa na wadunguaji yani snipers.

Labda tuseme aliyemshambulia Trump ni learner kwenye kutumia bunduki kwa sababu ni kijana wa miaka 20 tu tena kijana wa elfu mbili aitwaye Thomas Matthew Crooks, kijana kutokea Jimbo la Pennysylvania.

Mkasa mzima upo hivi

Eneo la Butler, Pennsylvania Jumamosi Julai 13 2024, Jioni aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump, alishambuliwa akiwa katika mkutano wa hadhara lakini pia mtu mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya.

Saa 6:05:12 p.m. Kwa majira ya marekani Trump alianza kuhutubia watu waliojitokeza uwanjani, na alizungumza kwa takribani dakika sita kabla mambo hayajawa mvurugano.
Wakati akihutubia ilisikika sauti ya mtu ikisema “He’s got a gun” akimaanisha yupo na bunduki, kisha ikasikikia sauti ya mtu mwingine kwenye umati huo akisema “Juu ya paa yupo na bunduki”, baada ya hapo ikasikika milio mitatu ya risasi kisha ikatulia na baadae ikasikika mingine mitano.

Baada ya hapo Ikasikika sauti ya mhudhuriaji wa mkutano ikisema “kaa hapa” “He’s got a gun ameshika bunduki kisha baadae .“Stay under here” kaa chini hapa saa kumi na mbili na dakika 11 Trump alikatisha kuzungumza sentensi aliyokuwa akizungumza kisha akashika sikio la upande wa kulia.

Baada ya tukio hili Tump alizingirwa na walinzi wa siri(secret agents) waliopanda kwenye jukwaa haraka huku wakisema “kaa chini kaa chini” Umbali kutoka kwa mlengaji hadi alipo Trump ilikuwa takribani hatua mia nne mpaka hatua mia tano.
Trump aliendelea kubaki chini akiwa amezingirwa na walinzi huku sauti zao zikisikika kupitia kipaza sauti cha kuhutubia wakisema mlengaji kashaangushwa, baada ya hapa askari na wanausalama wakajaa kwenye stage.

Saa 6:11:41 p.m. Agent wa kike akawa anasema “tunafanyaje” ikionyesha akiwa kwenye taharuki. Kwa mbali ikasikika sauti ya mtu akilia kwa uchungu ambapo sauti hii ni ya mwanamke, sauti ilitoka baada ya mlio wa risasi kusikika.
Baadae ikasikika sauti ya mlinzi wa kiume ikiwaambia wenzie nenda kwenye spare (akimaanisha magari aina ya Limousine ambayo ni magari maalum ya kumbebea rais au watu maalum na muhimu).

Baada ya hapo Ikasikika sauti ya mlinzi mwingine ikisema twende kwenye spare, subiri, subiri ukiwa tayari, kwako kisha mlinzi mmoja akasema twende ikiruhusu waondoke Wakainuka baada ya amri ya kutoka zikafanyiwa kazi kisha wakaanza kutoka.

Secret agents ili waweze kuondoka kama wako na mtu wanamlinda wakati wa kuondoka inapaswa eneo zima liwe salama na hapa ikasikika kauli “Hawkeyes here” Hawkeeye ni code ikimaanisha timu ya ushambulizi wa haraka imefika na ukitazama kwenye video utaona askari wenye silaha za kutosha wao binafsi wakiwa na mavazi ya kijeshi wamejaa katika eneo la karibu na anapohutubia Trump baada ya timu hii kufika ndipo ikaanza kumtoa.

Askari wa kike akauliza tupo sawa? Wakajibu tupo sawa tuondoke Walinzi wakamuinua trump ili kumshusha kwenye stage lakini aliposimamishwa ni dhahiri shahiri sikio lake la kulia lilikuwa linadondosha damu ambayo imechuruzika mpaka eneo kiasi la uso. Asili ya trump ni ubishi baada ya kusimamishwa ili atoke yeye alikunja ngumi na kurusha mkono juu huku akisema pambaneni, pambaneni, yani “fight fight” takribani mara tatu.

Inawezekana wakati ameinamishwa chini ili kumpa walimvua viatu kwani wakati anaondoka hapa alikuwa anawaambia walinzi “wacheni nichukue viatu vyngu” mlinzi wa kiume akamjibu nimekupata nimekupata, lakini Trump alisisitiza kupata viatu vyake, hapa mlinzi mwingine ikabidi kumkumbusha kuwa asubiri kwani anatokwa na damu eneo la kichwani.

6:12:54 zoezi la kumtoa trump jukwaani na kumuokoa lilikuwa limekamilika.

Yapata takribani dakika 40 baada ya yeye kuokolewa taarifa kutoka kwa msemaji wake ilikuwa ikisema Trump yuko sawa na anaendelea kuangaliwa afya yake.

Baadae msafara wake ulionekana kutokea katika hospitali ya Butler Memorial Hospital ambapo alienda kupata msaada wa kwanza na matibabu pia kuhakiki afya yake. Mapema Jumapili Julai 14 2024 Trump alirudi Newark, Jimbo la New Jersey baada ya kutoka Pennsylvania.

Huku Naibu mkurugenzi wa Mawasiliano ya Trump Caroline Sunshine, akipost video katika mtandao wa X na kuandika “Imara, amerudi katika ubora na hatoacha kuipigania marekani”.

Baadae kupitia ukurasa rasmi wa Donald trump katika mtandao wa Truth alipost na kuandika ,

“Nataka niwashukuru walinzi wa siri wa marekani, vyombo vya ulinzi na usalama, kwa muitikio wao wa haraka kwenye tukio la kupigwa risasi eneo la Butler Pennsylania. Muhimu zaidi nataka nitoe salam za rambi rambi kwa familia ya mtu mmoja aliyeuawa na familia ya mtu mmoja aliyejeruhiwa vibaya. Inasikitisha kitendo kama hicho kutokea katika nchi yetu. Kwa wakati huu hakuna kinachojulikana juu ya mfyatuaji wa risasi aliyefariki. Nilipigwa na risasi ambayo imechana eneo la juu la sikio langu la kulia, nilijua haraka kitu hakipo sawa niliskia “Whizzing sound” hizi ni sauti kama ulishawahi kupigwa sikio, nikasikia milio ya risasi na risasi ikakata ngozi yangu. Damu nyingi ilianza kumwagika hivyo nikafahamu nini kimetokea.

Akamaliza kwa kuandika God Bless America yaani Mungu ibariki Amerika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!