Latest Posts

GERSON MSIGWA: NEEMA NA MAENDELEO YA WATANZANIA YANAVUTIA MAADUI

Kulingana na Msemaji Mkuu wa serikali ya Tanzania Bw. Gerson Msigwa, hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa nchini pamoja na uwekezaji unaoendelea kufanywa na serikali umekuwa neema kwa Watanzania na kuvutia maadui wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi, akitoa wito kwa Watanzania kutorubuniwa na kuwa sababu ya kuharibu bidii zao wenyewe pamoja na neema hiyo ya maendeleo.

Gerson Msigwa amebainisha hayo wakati wa mahojiano yake na Kituo kimoja cha habari Jijini Dar Es Salaam, akieleza kwamba;

“Nchi yetu kwasasa hivi inaenda kwenye uchumi mkubwa wa gesi, nchi yetu sasa hivi inaenda kwenye uchumi mkubwa wa madini adimu, tunaenda pia kwenye uchumi mkubwa utakaotokana na uwekezaji wetu kwenye bandari zetu za Dar Es Salaam na Bandari ya Bagamoyo ambayo tunaanza Kuijenga.

“Uchumi wetu utakwenda kuchochewa kwa kiasi kikubwa na miradi yetu mikubwa; SGR ambayo inachanja mbuga na tayari tumeanza kujenga njia ambazo zitakwenda mpaka nchi jirani. Nchi yetu inaenda kwenye uchumi mkubwa utakaosaidiwa na nishati ya umeme.”

“Haya mambo yanaleta neema na pia yanavutia maadui. Ni vizuri Watanzania wawe macho, tusikubali kuchoma nchi yetu, kubomoa nchi yetu hasa kipindi hiki ambacho tunaelekea kwenye neema kubwa na serikali ipo tayari kutufikisha kwenye neema kubwa.” Amesema Bw. Msigwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!