Latest Posts

HII NDIYO IDADI ILIYOFICHWA YA WALIOFARIKI KENYA KWENYE MAANDAMANO

Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu nchini Kenya (KNCHR) imesema idadi ya waliofariki dunia imefikia 39 huku 361 wakijeruhiwa tangu kuanza kwa maandamano ya kupinga mswada wa Fedha 2024 kote nchini humo.

Taarifa iliyotolewa Jumatatu Julai 01, 2024 na Mwenyekiti wa tume hiyo Roseline Odede imeeleza kuwa idadi huenda isiwe kama ilivyoelezwa kwani uchunguzi wa maiti kwa wengi wa waathiriwa bado haujafanywa.

Tume ya KNCHR pia imesema kumekuwa na taarifa za watu 32 kutekwa nyara na 627 kukamatwa kiholela huku baadhi ya watu wakisemekana kuwa mafichoni kutokana na vitisho dhidi ya maisha yao na watu wasiojulikana.

Katika ripoti yake, Tume hiyo imeendelea kushutumu utumiaji wa nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji na wengineo kama wafanyakazi wa afya, waandishi wa habari na kwenye maeneo salama kama vile makanisa na vituo vya dharura vya matibabu.

Hata hivyo Rais William Ruto siku ya Jumapili, Juni 30, wakati wa kikao na wanahabari, alisema kufikia wakati huo waliofariki walikuwa 19 huku akiongeza kuwa maafisa wa polisi walitekeleza majukumu yao kwa njia huru wakati wa maandamano hayo.

Kufuatia maandamano ya siku nzima ya kupinga Muswada wa Sheria ya Fedha mnamo Jumanne, Juni 25, ripoti ambazo hazijathibitishwa ziliibuka kwamba polisi na vikosi vya kijeshi vilikuwa vikiwachinja watu katika eneo la makazi usiku wa manane.

Katika kikao cha wanahabari katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumapili, Ruto aliulizwa kuhusu idadi ya watu waliouawa na polisi tangu kuanza kwa maandamano, ambayo alishikilia msimamo wake kuwa kuwa ni 19 lakini mashirika ya kutetea haki ikiwa ni pamoja na KNCHR yameweka namba hiyo kuwa juu zaidi.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani tayari maandamano yameanza katika maeneo kama vile Mombasa licha ya Rais Ruto kutangaza Jumatano iliyopita kwamba hatatia saini Muswada tata wa Fedha kuwa sheria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!