Latest Posts

IKULU ZANZIBAR YAWARUKA WALIOSEMA RAIS AONGEZEWE MIAKA 7 “JAMBO HILI HALINA TIJA KWA NCHI YETU”

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Idara ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imepinga vikali maoni yaliyotolewa hivi karibuni ya kupendekeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba badala ya miaka mitano iliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar.

Kulingana na taarifa iliyotolewa Jumatatu Juni 24, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar Charles Hilary, imeelezwa kuwa maoni hayo hayana tija wala faida kwa nchi ya Tanzania na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachotajwa kufuata misingi ya demokrasia.

“Rais Dk. Mwinyi ni muumini wa kufuata Katiba na Sheria za nchi, tunapenda kusisitiza kwamba maoni haya si ya Mhe. Rais wala sio ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar. Kwa muktadha huu, Rais Dk. Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano” Imeeleza taarifa hiyo.

Kulingana na Hilary, Rais Mwinyi amewasihi wale wote wenye mawazo tofauti na hayo wafunge mjadala huo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!