Latest Posts

‎JACKSON KANGOYE AFUNGUKA KUHAMIA ACT  WAZALENDO NA KUCHUKUA FOMU

Na Helena Magabe ,Tarime.

‎‎Jackson  Ryoba Kangonye aliyekuwa Kada wa chama cha mapinduzi (CCM)  na mtia nia  Ubunge jimbo la Tarime Mjini  kupitia chama hicho,anehamia ACT Wazalendo ambapo amechukua fomu na kurejesha ili kuwania Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini.

‎Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kurejesha fomu  ofisi za Tume huru ya uchaguzi katika Halmashauri ya Mji Tarime , amesema kuwa ameamua kuhamia ACT Wazalendo kwa utashi wake, hivyo endapo Tume itaridhia na kumpa ridhaa ya kugombea kupitia chama hicho atashinda kwa kishindo kwani ana upepo wa kushinda kwani yeye ndio tamanio la Wabanchi.

‎Amesema kuwa amekitumikia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa muda mrefu akatia nia kugombea Ubunge 2020 akaongoza kwa kura za maoni lakini jina lake halikuteuliwa ,ametia nia kwa mara nyingine 2025 Wajumbe wakampitisha na  kuwa mtu wa pili kulingana na chama kuwa na matakwa yake na utaratibu wake ameona maoni ya Wajumbe ambao ni wengi hayakufanyiwa kazi hivyo ameamua kuwa sehemu ya wale ambao hawakusikilizwa, kwani anaona ni kama wamedhalilishwa hivyo kwa utashi wake na akili timamu amehamia ACT Wazalendo akawasemee Wananchi huko.

‎Kangonye  amesema kilichofanyika ni ubadhirifu lakini atashinda kupitia Ubunge kupitia ACT Wazalendo na si kwamba atakuwa Mbunge tu ,bali ni kwa sababu ya kulisemea Jimbp la Tarime Mjini na Mlango mmoja ukifungwa,  unafunguliwa hivyo mlango wa CCM umefungwa lakini wa ACT Wazalendo umefunguliwa hivyo haoni Mgombea jimbo la Tarime mjini atakayeshinda.

‎”Aliyepitishwa sijaona kitu kipya alichonacho  atakachoweza  kushawishi wananchi  kwa miaka 15 aliyokuwa Mbunge lakini Mimi  nina mapya mengi na Mimi  ndio tamanio la Wananchi wa Tarime Mjini” Alisema Kangoye

‎Aidha amesema lengo lake kubwa la  kuwa Mbunge  nikutaka nikuzuia rasimali za Wananchi zisitumike vibaya zibaki kwa Wananchi wenyewe,na kuongeza kuwa Wananchi wanahitaji miundombinu bora, mfano maji ,shule ,Hosipitali na mambo mengi muhimu ambayo wanayakosa na Yeye anaona anatosha kuwapambania wananchi wa Tarime mjini kwa mapungufu hayo.

‎Hata hivyo amesema akifanikiwa kuwa Mbunge atabana matumizi makubwa ya ghalama za Serikali ili yaweze kuwa na uwiano wa kodi kwa Wananchi na kuongeza kuwa Watu wa kada ya chini hawanufaiki na mkopo wa asilimoa 10 unabaki kwenye makaratasi hayo ni mambo kufatilia akiwa Mbunge.

‎Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Charles Mwera ambaye amewahi kuwa Mbunge kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) amechukua na kurejesha fomu ya Ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia ACT Wazalendo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!