Latest Posts

KATAMBI NA MATUKIO YA OKT.29: SHERIA NI MSUMENO, HAKUNA ATAKAYESALIMIKA KWENYE TUME ZA RAIS

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa watu waliohusika na vurugu za Oktoba 29, 2025 akisisitiza kuwa serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haitampendelea mtu yeyote katika kutoa haki.

Akizungumza jana katika Kijiji cha Kangagani, Kaskazini Pemba, alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuweka jiwe la msingi la Skuli ya Amali inayojengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 4, Waziri Katambi ametolea ufafanuzi juu ya tume zilizoundwa na Rais kuchunguza vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 29. Amebainisha kuwa kuundwa kwa tume hizo ni hitaji la sheria za kitaifa na kimataifa ili nchi ianze kuchukua hatua yenyewe

Waziri Katambi ameeleza kuwa baada ya Tume ya Jaji Chande kukamilisha kazi ya kutafuta ukweli, sasa Tume ya Jaji Lila imeanza kazi ya kushughulikia masuala ya kijinai. Katika kusisitiza msimamo wa serikali kuhusu usawa mbele ya sheria, Waziri Katambi amesema,

“Ndugu zangu Watanzania niwaambie na niwahakikishie serikali iko very serious na jambo hili. Hatutapendelea mtu, hata kama ni Katambi anahusika atawajibika. Sheria ni msumeno. Yeyote ambaye anahusika… awe kiongozi wa serikali, awe ni kiongozi mtu binafsi, awe yoyote, awe ni raia aliyehusika katika changamoto hizo tulizokwenda kuzipata, atawajibika kwa mujibu wa sheria”

Aidha, Waziri Katambi aligusia kuwa upinzani unaojitokeza dhidi ya tume hizo unatokana na watu waliohusika na vitendo hivyo kuhofia ukweli utakaobainika. Alisisitiza kuwa sheria itafanya kazi yake kwa wahusika wote, wawe ni watendaji wa serikali (state actors) au watu binafsi (non-state actors), ikiwemo wale waliofadhili au kuchochea vurugu hizo kwa namna yoyote

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!