Latest Posts

NAIBU WAZIRI QWARAY AWATAKA WAAJIRI KUACHA UTENDAJI WA MAZOEA.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, ametoa maelekezo kwa waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu, akiwataka kuhakikisha changamoto za kiutumishi zinashughulikiwa kwa wakati ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia sheria, maadili, usawa na uwajibikaji.

‎Qwaray ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kazi cha kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.

‎

‎Ameagiza waajiri kuhakikisha stahiki za watumishi, ikiwemo kupandishwa vyeo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara na mafao, zinashughulikiwa kwa wakati, huku madai ya watumishi yakihakikiwa na kuwasilishwa yakiwa na nyaraka muhimu.

‎ Aidha, Qwaray amezitaka Mamlaka za Ajira na Nidhamu kusimamia haki na wajibu wa watumishi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma na kuacha utendaji wa mazoea.

‎

‎Kuhusu maadili,  Qwaray amewataka watumishi kuyafahamu na kuyatekeleza kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma, “Watumishi wanaokiuka maadili au kutotekeleza majukumu yao ipasavyo wanapaswa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu kwa wakati.”

‎Aidha, amewataka waajiri na Mamlaka za ajira na nidhamu kushirikiana na tume ya Utumishi wa Umma katika ukaguzi wa utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi na kurekebisha mapungufu yatakayobainika kwa wakati.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!