Latest Posts

MWISHO WA MGOMO WA MABASI: WAZIRI MKUU DKT. NCHEMBA AKUTANA NA MADEREVA, MGOMO WA SIKU MBILI WASITISHWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Septemba 30, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo maalum na viongozi wa madereva wa mabasi na malori nchini katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo umefanyika kufuatia mkwamo uliotokana na mgomo wa madereva uliodumu kwa siku mbili mfululizo katika baadhi ya mikoa nchini, uliovuruga shughuli za usafiri wa umma na kuwaacha abiria wakiwa wamekwama vituoni.

Katika mazungumzo hayo yaliyolenga kutafuta suluhu ya kudumu, viongozi wa madereva wameafiki kusitisha mgomo huo ili kuruhusu huduma za usafiri na usafirishaji kurejea kama kawaida, huku Serikali ikisisitiza utayari wake wa kusikiliza, kuchambua, na kuzifanyia kazi changamoto zote zinazowakabili wadau hao wa sekta ya usafiri nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!