Latest Posts

TRA YAFICHUA NJIA RAHISI YA KUTAMBUA BIDHAA BANDIA

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa rai kwa wananchi kuhakiki stempu za kielektroniki kwenye bidhaa wanazonunua kabla ya kuzitumia, ili kuepuka kutumia bidhaa bandia na zisizokidhi viwango vya ubora.

‎Rai hiyo imetolewa na Kaimu Meneja wa   TRA Mkoa wa Dodoma, Aubrey Silayo leo Novemba 17,2026 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu   matumizi ya mfumo wa stempu za kodi za kielektroniki kwenye vinywaji na bidhaa nyingine.

‎Amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa inamwezesha mtumiaji kutambua bidhaa halali zinazokidhi viwango vya ubora na matakwa ya kisheria, huku ikisaidia kubaini bidhaa bandia au zisizothibitishwa usalama wake na mamlaka husika, hivyo kulinda afya za wananchi.

‎Aidha, Silayo amewataka watengenezaji, waagizaji na wauzaji kuhakikisha bidhaa wanazoziingiza sokoni zinakuwa na stempu sahihi za kielektroniki na kuongeza kuwa matumizi ya stempu za kughushi ni kosa la kisheria na kwamba TRA inatumia mifumo ya kiintelijensia pamoja na skana maalumu kubaini vitendo hivyo.

‎Ameonya kuwa watakaobainika wanaweza kutozwa faini ya Sh milioni tano hadi milioni 50, kifungo kisichozidi miaka mitatu au adhabu zote mbili, akisisitiza kuwa kuhakikisha bidhaa zinatumia stempu halali ni jukumu la kila mmoja.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!