Latest Posts

WAFUGAJI SANGASANGA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI WA MILIONI 65

 

Wafugaji wa Kijiji cha Sangasanga, Kata ya Mzumbe, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, wanatarajia kunufaika na mradi wa maji safi na birika la kunyweshea mifugo, utakaosaidia kulinda vyanzo vya maji na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji kwa matumizi ya nyumbani na mifugo katika eneo hilo na vijiji jirani.

Akikabidhi mradi huo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira mkoani Morogoro, iliyolenga kukagua utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 65, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Patrick Mwalumenge, amesema mradi huo utasaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Sangasanga.

Kwa upande wao, baadhi ya wafugaji wa jamii ya Kimasai ambao ni miongoni mwa wanufaika wa mradi huo, kupitia kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiegea, Karangushyo Akiro, wamesema kukamilika kwa mradi huo ni faraja kwao kwani kutawapunguzia adha ya kutafuta maji kwa ajili ya mifugo yao.

Akizungumzia gharama za mradi huo, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmassy, amesema bodi hiyo imetumia shilingi milioni 65 kutekeleza mradi huo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kusogeza huduma ya maji kwa jamii na kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!