Theophilida Felician Kagera.
Chama cha ACT WAZALENDO kimesikitishwa na changamoto zinazowakabili wafanya biashara ndogondogo machinga Bukoba na kwingineko nchini ambako kimeapa kuchukua hatua mahakamani.
Hayo yamebainishwa na Naibu waziri mkuu kivuli wa ACT Mhe Luhaga Joelson Mpina akiwahutubia wananchi wa kata ya Kikomero jimbo la Bukoba vijijini mkoani Kagera 5,Novemba 2026.
Miongoni mwachangamoto hizo Mpina amezitaja kuwa nipamoja na suala la kuwaondoa machinga maeneo yao ya awali mjini Bukoba nakuwahamishia maeneo yasiyo rasmi na wezeshi kwaugumu wakuwapata wateja jambo ambalo limewapelekea biashara kudorora hadi kupoteza mwelekeo wa kufanya kazi huku wakikabiliwa na madeni rukuki ya mikopo hususani ya Benki, kupoteza mitaji yao na hali ngumu ya kimaisha.
Amefafanua kwamba kutokana na hali hiyo tayari ACT itachukua hatua ya kuwaagiza machinga wote nchi nzima kujiorodhesha kwa ajili ya kuungana na chama hicho ili kuchukua hatua mahakamani kupinga hali hiyo ambayo ameitaja kuwa ya unyanyasaji.

Hata hivyo kiongozi huyo nawenzake akiwemo makamu ACT Isihaka Mchinjita awali walisimama baadhi ya maeneo ya Bukoba mjini nakusalimia wananchi amewasihi kuungana na ACT kushinikiza mambo kadhaa ikiwemo kutungwa kwa katiba mpya na kuachiwa huru watuhumiwa wakisiasa walioko magerezani.
Naye makamu wa ACT Bara, Isihaka Mchinjita alisema kuwa changamoto kwa machinga zinasababishwa na kukosekana kwa sera madhubuti zenye kuwawezesha ipasavyo jambo ambalo halileti tija kwa vijana na makundi ya akina mama wanaopambana kujikwamua na umaskini kupitia shughuli hiyo.
Hata hivyo viongozi hao wametoa wito kwa madiwani 65 wa ACT nchini kuhakikisha wanasimama imara na kuhoji mamlaka pale wanapobaini uwepo wa mambo yenye kuwanyanyasa wananchi kwa lengo la kushughulikiwa.
Kwingineko Kiongozi Mpina ametawazwa rasmi kuwa kiongozi wa kimila wa wahaya kutoka kwa viongozi wa kimila Bukoba walioshiriki matukio mbalimbali yaliyowaongoza kufanikiwa zoezi hilo.
