Latest Posts

MGOGORO WA ARDHI WA MIAKA 36 WAFIKIA MWISHO, KANISA KATOLIKI LAACHIA WANANCHI EKARI 35.7 BUGANJO

 

Na Helena Magabe,Rorya

Kanisa Katoriki jimbo la Musoma liliamua  kuwachia Wananchi eneo walilovamia  lenye ukubwa wa ekari 35.7 huku likiwaomba eneo lililobaki lenye ukubwa wa ekari 51.16 wasilivamie kwani mikakati ya kuliendeleza imekamilika.

Kijjiji cha Buganjo kata ya Bukwe Wilayani Rorya kinadaiwa kuvamia eneo la kanisa katoriki lenye ukubwa wa ekari 35.7 na kusababisha mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 36 ambapo kanisa limeaamua kuwaachia mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Rorya  Stanslauce Mabula  ameshukuru juu ya hatua hiyo.

Kwa mujibu wa Padre Michael Nyamuhanga ambaye ni   katibu msaidizi wa Baba Askofu na aliyekuwa  Mwakilishi wa bodi ya
udhamini alimwambia Dc Mabula kuwa  eneo hilo linamilikiwa na kanisa kwa hati namba 8148  lenye ukubwa wa ekari 91  na wakati kanisa inalimiliki hakukuwana makazi ya  Watu  kwani wangekuwepo wangetakiwa kulipwa fidia.

Aliongeza kuwa   baadaa ya Wananchi kuvamia eneo lenye ukubwa wa ekari 35.7  kanisa lilikuwa likitumia ekari 4.3  hivyo wananchii wametakiwa kutovamia eneo ambalo limebaki lina ukubwa wa  ukubwa wa ekari 51.16.

Alisema haikuwa rahisi kuwaachia kwani kuvamia eneo ni kinyume na Sheria  ya mwaka 1999 kifungu no 175 lakini waliamua kuachia kwaajili ya kujenga mahusiano mazuri .

Hatua hiyo imemfurahisha Dc wa  Wilaya hiyo  kwa uamuzi huo ambapo alipongeza kanisa kwa kutatua mgogoro huo uliodumu miaka mingi  na kuongeza kuwa upo mgogoro mwingie katika Wilaya yake baina ua Kanisa na Wananchi.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!