Na Helena Magabe-Tarime
Hatimaye Julai 5, 2025 Shomari Binda aliyekuwa Mwandishi wa Habari Mkoani Mara alipumzishwa kwenye nyumba yake ya milele Musoma mjini alipokuwa akiishi baada ya kifo chake kutokea Julai 3, 2025 katka hospitali ya rufaa ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere(Kwangwa ) Musoma alipokuwa akipatiwa matibabu.
Binda aliyekuwa nguli wa habari za michezo niliyewahi kufanya nae field katika redio ya Victoria Fm iliyoko Musoma alikuwa mahiri kwenye habari za michezo na mchambuzi mzuri kwenye mpira wa miguu alikuwa akifaya kipindi cha michezo, alikuwa na kipaji kingine cha kutunga mashairi na kuimba kwa umahiri mkubwa ,kabla ya kifo chake alikuwa akiandikia vyombo mbalimbali na alijitika zaidi kwenye blog ya George Marato.

Enzi za uhai wake alikuwa akishiriki katika shughuli mbali mbali za kitasnia na nyinginezo na pale alipopata nafasi ya kuimba shairi hakika alikuwa akikutaja ni lazima utanyanyuka kumtuza ,binasfi iliwahi kunitokea ndio maana imeniwia ngumu kuacha kukumbuka walau alama aliyoicha Binda kwa kuimba na kwenye tasnia ya Habari Mara.
Nguri huyo aliyewaliza waandishi wa habari wengi atakumbukwa kwa upole na ucheshi wake, tangu nilipomfahamu Shomari aliyejiita shomy B pale Victoria Fm sina kumbukumbu kama niliwahi kumwona amekasilika au kusikia amekosana na Mtu ,tuliishi naye Vizuri baadaye tukakutana kwenye magazeti kisha tukahamia kwenye mitandao ya kijamii, tulikuwa tukishea mengi nakumbuka alivyokuja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Tarime kuna jambo aliniomba tulishea na akanishukuru akisema akisema asante Dada.
Katibu wa klabu ya Waandishi wa habari na Makamu wa Rais Umoja wa vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Pendo Mwakyembe kwa uchungu na maumivu anamkumbuka Binda kwa ucheshi,utani ,upole ,usikivu na mwenye kujichanganya na watu aliyewasemea Waandishi wenzake wa Mara kwa mazuri hata alipokuwa nje ya Mkoa wa Mara.
Alisema aliwahi kuwa kiongozi wake wa mpito akiwa Mwenyekiti na yeye akiwa katibu katika kipindi cha miezi sita 6 ambayo alifanya nae kazi kwa amani na furaha kwani kila alipotaka kufanya jambo alimpigia simu kutaka ushauri wanakubaliana kisha akaendelea na mambo yake,baadaye uchaguzi ulifanyika akawa Makamu mwenyekini na Mugini Jacob akawa Mwenyekiti.
Mwakyembe aliongeza kuwa wakati anagombea ujumbe wa bodi UTPC mwaka 2017 ,Binda alimwimbia shairi la kumnadi na kila alipopata nafasi alimwimbia kumnadi na hatimaye alimwimbia mbele ya mkutano mkuu na kunadi sifa zake kwa wajumbe wa mkutano mkuu mpaka ukumbi mzima ukalipuka kwa shangwe,
Alitaja sifa zake nyingi lakini vile vile waandishi mbali mbali Mkoani Mara kwa nyakati tofauti wamesimulia mazuri ya Binda aliyekuwa nguri wa habari za michezo na nyinginezo pia msanii wa mashairi ,klabu mbali mbali Nchini zimetoa salamu za rambirambi kwa klabu ya Mara huku Waandishi wa habari wa Mara tukibaki na funzo juu ya kuishi vizuri na Jamii ,Binda kipenzi cha wengi umevipiga vita vilivyo vema mwendo umeumaliza lala salama.