Latest Posts

KILOMITA 33 ZA LAMI KUWANUFAISHA WANANCHI IRINGA KUPITIA MRADI WA RISE

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inaendelea na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwenye barabara za Wenda-Mgama (Kilomita 19) na Mtili-Ifwagi (Kilomita 14) katika wilaya za Iringa na Mufindi, mkoani Iringa ambazo ni sehemu ya Mradi wa Uboreshaji wa Barabara Vijijini kwa Ushirikishaji wa Jamii na Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE).

Meneja wa TARURA Wilaya ya Mufindi, Mhandisi Richard Sanga, ameeleza kuwa barabara hizo zitasaidia wananchi katika shughuli za kilimo na biashara, akisema: “Kukamilika kwa barabara ya Mtili-Ifwagi kutaiwezesha Wilaya ya Mufindi kufikisha jumla ya kilomita 87.3 za barabara za lami, na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa wananchi.”

Aidha, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa RISE, Mhandisi Joel Mwandobo, ameeleza kuwa ujenzi wa barabara hizo unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2025, huku akitoa wito kwa mkandarasi, kampuni ya CHICO, kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa mujibu wa ratiba.

Mradi wa RISE unatekelezwa na TARURA katika mikoa ya Iringa, Geita, Tanga, na Lindi, ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya barabara ili kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!